- Familia ya Spika wa Bunge la Seneti Amason Kingi imetumbukia kwenye majonzi kufuatia kifo cha babake Mzee Kingi Mwaruwa
- Msemaji huyo alibainisha kuwa walicheza kwa furaha na babake Siku ya Krismasi bila kujua kwamba itakuwa mara yao ya mwisho kucheza dansi
- Rais William Ruto, Mawaziri Hassan Joho na Kipchumba Murkomen pamoja na viongozi wengine pia wameshiriki pongezi zao
Spika wa Bunge la Seneti Amason Kingi ametoa ujumve wa kumuenzi na wa moyoni kwa babake marehemu Mzee Kingi Mwaruwa akimtaja kuwa nguzo ya nguvu na ustahimilivu.
Chanzo: Facebook
Amason Kingi amlilia baba yake
Katika ujumbe wa hisia kali siku ya Jumapili, Februari 9, Kingi alikumbuka tukio maalum waliloshiriki wakati wa Krismasi mnamo Desemba 25, 2024, katika kijiji cha Mjanaheri, ambapo walicheza pamoja kwa mara ya kwanza—na ambayo pia ikawa ya mwisho.
“Tangu nilipofikia utu uzima, sikumbuki tukiwahi kucheza pamoja, baba. Lakini siku ya Krismasi, kwa mara ya kwanza kabisa, tulicheza, tukafurahia na kujivinjari. Uso wako ulionekana kung’aa kwa furaha. Hatukuwa tu tukisherehekea Krismasi bali tulikuwa tukimshukuru Mwenyezi Mungu kwa nafuu yako baada ya miaka mingi ya kupambana na maradhi mbalimbali. Sikujua kuwa huo ungekuwa mdundo wetu wa kwanza na wa mwisho,” Kingi alieleza kwa masikitiko.
![](https://cdn.tuko.co.ke/images/360x203/6d2afdefa343b6e3.jpeg?v=1)
Pia soma
Magazeti ya Kenya: Jinsi hatua ya Ruto Kaskazini Mashariki mwa Kenya itabadilisha kura ya 2027
Spika wa Seneti alitafakari kuhusu kujitolea kwa babake na changamoto alizopitia ili kumkuza, akimshukuru kwa kumpatia somo la thamani la uvumilivu.
“Nimevunjika moyo kabisa, baba, hasa ninapokumbuka safari yenye maumivu na mapambano uliyopitia ili kuniunda kuwa mtu niliye leo. Ulinifundisha masomo mengi ya thamani, kubwa zaidi ikiwa ni kutokata tamaa, haijalishi changamoto zinavyokuwa ngumu. Ni funzo hili limenifikisha hapa nilipo,” aliandika.
Kingi alihitimisha heshima zake kwa babake kwa ujumbe wa kugusa moyo, akitumai kuwa babake atapokelewa mbinguni kwa furaha ile ile waliyoishiriki wakati wa densi yao ya mwisho.
“Baba, na malaika wafungue Milango ya Mbinguni na wakukaribishe kwa densi, kama tulivyofanya kule Mjanaheri. Mpaka tukutane tena, Baba.”
Viongozi wangapi wameomboleza kifo cha baba yake Kingi?
Kifo cha Mzee Mwaruwa kimewaacha Spika na familia yake katika maombolezo makubwa, huku rambirambi zikiendelea kumiminika kutoka kwa viongozi na Wakenya kote nchini.
Rais William Ruto aliomboleza:
“Rambirambi zetu kwa Spika wa Seneti kwa kumpoteza babake mpendwa, Mzee Kingi Mwaruwa. Alikuwa mtu mwenye heshima, mwenye maendeleo na mchapakazi. Mheshimiwa Amason Kingi, familia na watu wa Kilifi mpo katika maombi yetu katika wakati huu mgumu. Pumzika kwa amani.”
Aisha Jumwa alisema:
“Mawazo na maombi yangu yako pamoja na Rt. Hon Amason Jeffah Kingi EGH, Spika wa Seneti, kufuatia kifo cha baba yako mpendwa, Mzee Kingi Mwaruwa.
Na upate nguvu na neema kustahimili pigo hili, na Mwenyezi Mungu ampe Mzee pumziko la milele.”
Mbunge Didmus Barasa alisema:
“Rambirambi zetu za dhati kwa Spika wa Seneti Rt. Hon Amason Jeffah Kingi EGH, familia yake, na watu wa Kilifi kwa kumpoteza baba mpendwa, Mzee Kingi Mwaruwa; mtu wa busara, uadilifu, na muungwana. Katika kipindi hiki cha huzuni, tunasimama na Mheshimiwa Kingi na familia yake katika maombi. Mungu awape nguvu na faraja katika wakati huu mgumu. Pumzika kwa amani, Mzee Kingi Mwaruwa.”
Waziri CS Ali Hassan Joho alisema:
“Ninatoa rambirambi zangu za dhati kwa kaka yangu, Spika wa Seneti Rt. Hon. Amason Jeffah Kingi kufuatia kifo cha baba yako, Mzee Kingi Mwaruwa. Mwenyezi Mungu akufariji na akupe nguvu kuvumilia msiba huu mkubwa.”
![](https://cdn.tuko.co.ke/images/360x203/b219bb5c38278654.jpeg?v=1)
Pia soma
Leonard Mambo Mbotela: Wakenya waomboleza baada ya mtangazaji mkongwe kutupa mkono wa buriani
Waziri Kipchumba Murkomen aliandika:
“Rambirambi zangu za dhati kwa Spika wa Seneti, Rt. Hon Amason Jeffah Kingi EGH na familia nzima, kufuatia kifo cha baba yao mpendwa, Mzee Kingi Mwaruwa. Mawazo na maombi yetu yako pamoja nawe, ndugu yangu, familia yako, na watu wa Kilifi, katika wakati huu mgumu wa maombolezo. Hakika, sisi ni wa Mungu, na kwake tutarejea.”
Read ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.
Chanzo: TUKO.co.ke