Mnamo Jumatatu, Februari 10, magazeti ya kitaifa yaliripoti kwa mapana kuhusu mauaji ya kutatanisha ya Gibson Kinyua, ambaye alipatikana amefariki ndani ya wadi katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta.
Chanzo: UGC
1. The Standard
Chapisho hilo liliripoti kuhusu kifo cha kutatanisha cha Gibson Kinyua, mgonjwa aliyepatikana ameuawa ndani ya wadi katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta (KNH).
Ripoti ya polisi ilithibitisha kuwa mwili wa Kinyua ulikutwa Ijumaa, Februari 7 saa kumi na mbili asubuhi wakati wa ukaguzi wa kawaida wa wadi. Kisu kilichojaa damu baadaye kilipatikana juu ya paa, kikishukiwa kuwa silaha ya mauaji.
Ripoti za awali zilidai kuwa muuaji huenda alikuwa mgeni aliyepenya hospitalini, kumuua mgonjwa kisha kutoweka.
Hata hivyo, kaimu Mkurugenzi Mkuu wa KNH, William Sigilai, alikanusha madai kuwa mshukiwa alikuwa mtu wa nje.
Sigilai alibainisha kuwa kwa sasa hakuna ushahidi wowote unaoonyesha kuwa mtu kutoka nje aliingia wodini kutekeleza mauaji hayo, lakini alithibitisha kuwa uhalifu huo ulifanyika na kisu, kinachodhaniwa kuwa silaha ya mauaji, kilipatikana.
![](https://cdn.tuko.co.ke/images/360x203/179bc895bcac84e2.jpeg?v=1)
Pia soma
Kirinyaga: Jamaa aliyeumizwa nyeti akidai deni la KSh 50 afunguka, ataka mhusika naye asikie uchungu
“Ningependa kusema kuwa kwa wakati huu hatuna ushahidi kuwa mtu yeyote aliingia na kutekeleza uhalifu huu. Hata hivyo, tunajua kwa hakika kuwa mgonjwa huyo aliuawa wodini. Tumeikabidhi kesi hii kwa Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI),” alisema Sigilai.
Sasa maafisa wa upelelezi wanajaribu kubaini jinsi muuaji alivyoingia wodini bila kunaswa kwenye CCTV na jinsi kisu kilivyojikuta juu ya paa.
Kizingiti katika uchunguzi ni kwamba kamera za CCTV za hospitali hazikufanya kazi wakati wa tukio hilo.
2. Daily Nation
Kiongozi wa chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka, amemshtumu Rais William Ruto kwa kuweka mikakati ya kuiba kura katika uchaguzi mkuu wa 2027.
Akizungumza Jumapili, Februari 9, wakati wa ufunguzi wa ofisi za chama cha Wiper Kilifi, Kalonzo alidai kuwa serikali ya Ruto inatumia mchakato wa usajili wa vitambulisho kama mbinu ya kudhibiti usajili wa wapiga kura katika maeneo fulani kuelekea uchaguzi ujao.
Aidha, alieleza kuwa kiongozi wa taifa anapanga kuwasajili raia wa kigeni kama wapiga kura ili kujihakikishia ushindi wa mapema mnamo 2027.
![](https://cdn.tuko.co.ke/images/360x203/467b73ec29e8da9c.jpeg?v=1)
Pia soma
Gilbert Kinyua: Mke wa mwanamume aliyeuawa KNH azungumza kwa uchungu, ataka muuaji akamatwe
Kalonzo alidai kuwa msukumo wa serikali wa kutoa vitambulisho katika maeneo maalum haukuwa hatua isiyo na nia bali ni mkakati wa kuathiri mchakato wa uchaguzi kwa manufaa ya Ruto.
Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa Wiper, mbinu hiyo imelenga kuongeza idadi ya wapiga kura katika baadhi ya maeneo huku maeneo mengine yakiachwa nyuma.
“Lazima tuwarudishe nyumbani mapema iwezekanavyo, na hakutakuwa na uwezekano wa wizi wa kura. Wanadhani wanaweza kuwasajili wapiga kura hapa na pale na kutoa vitambulisho vya taifa ili kuwasaidia katika njama yao,” alisema Kalonzo.
3. The Star
Gazeti hilo liliripoti kuhusu sababu zilizochangia uamuzi wa Chama cha Jubilee kumuidhinisha aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Ndani, Fred Matiang’i, kuwania urais.
Mipango ya kisiri inayodaiwa kufanywa na aliyekuwa naibu rais, Rigathi Gachagua, na kiongozi wa Wiper, Kalonzo Musyoka, kuhusu muungano wa 2027 ilisababisha Jubilee kumuidhinisha Matiang’i kama mgombea wao wa urais.
Katibu Mkuu wa Jubilee, Jeremiah Kioni, alidai kuwa wawili hao wamekuwa wakikipuuza chama cha aliyekuwa rais Uhuru Kenyatta katika mipango yao, ikiwemo kuingiza washirika wapya.
![](https://cdn.tuko.co.ke/images/360x203/6d2afdefa343b6e3.jpeg?v=1)
Pia soma
Magazeti ya Kenya: Jinsi hatua ya Ruto Kaskazini Mashariki mwa Kenya itabadilisha kura ya 2027
Mbunge huyo wa zamani wa Ndaragwa alisema kuwa chama cha Uhuru kiliwekwa pembeni baada ya yeye kupaza sauti kwamba upande wa upinzani ulikuwa unageuka kuwa “kona ya waliotimuliwa madarakani.”
Kioni aliongeza kuwa maonyo yake dhidi ya kuhusishwa kwa watu kama Gachagua, aliyekuwa gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu, na Mike Sonko katika siasa za upinzani hayakuzingatiwa.
Alidai kuwa Kalonzo na Gachagua wanapanga muungano wa kisiasa ambapo kiongozi wa Wiper atakuwa mgombea wa urais huku mgombea mwenza akiwa ama Gachagua au kiongozi wa Narc Kenya, Martha Karua.
“Kalonzo na Gachagua walikuwa wakisukuma mpango wa muungano bila kutushirikisha, ilhali sisi ni miongoni mwa vyama vikubwa ndani ya Azimio, kwa kweli hata kubwa kuliko Wiper,” alisema Kioni.
4. Taifa Leo
Gazeti la Kiswahili liliripoti kuhusu kukamatwa kwa vijana wasiopungua 43 kufuatia operesheni ya usalama katika kaunti ya Isiolo.
Kamishna wa Kaunti, Geoffrey Omoding, aliwaambia wanahabari siku ya Jumapili, Februari 9, kwamba polisi walikuwa wakiwalenga wauzaji wa dawa za kulevya, wanyang’anyi na wafanyabiashara wa pombe haramu katika kaunti hiyo. Watu waliokuwa wakizurura mjini baada ya usiku wa manane pia walikamatwa.
![](https://cdn.tuko.co.ke/images/360x203/01569308ee77bca8.jpeg?v=1)
Pia soma
USAID: Hofu yasambaa Huku Wakenya Wengi wakipoteza kazi kufuatia Donald Trump kusitisha ufadhili
Kwa mujibu wa kamishna wa kaunti, operesheni hiyo itaendelea kwa siku zijazo licha ya wimbi la ukosoaji kutoka kwa Wakenya mtandaoni kuhusu mazingira ya kukamatwa kwa vijana hao.
Kukamatwa kwao kulifanyika siku moja tu baada ya kundi la vijana kumzomea Rais William Ruto.
Read ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.
Chanzo: TUKO.co.ke